Pages

Pages

Thursday, August 08, 2013

Sikukuu ya Idd yaleta mkanganyiko, rasmi ni kesho sio leo


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAENEO ya Kimara, jijini Dar es Salaam, kumetokea mkanganyiko baada ya misikiti kuwa na mtazamo tofauti juu ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuipokea Sikukuu ya Idd.

Mtazamo huo pia upo katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi, hususan kutokana na imani kuamualiwa na watu wachache, hivyo kupoteza ladha na utetezi wa dini ya Kiislamu, hasa nyumba ile wanaswali na wale wanasubiri kesho kwa ajili ya kuusubiri mwezi hapo jioni ya leo.

Hata hivyo, idadi kubwa ya Waislamu wanaswali Sikukuu ya Idd kesho Ijumaa badala ya leo kama wanavyofanya baadhi yao.

“Sisi kwetu Idd itakuwa kesho Ijumaa, hivyo tunaomba waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea na mfungo mtukufu wa Ramadhan badala ya kusikiliza maoni ya watu wachache,” alisema sheikhe mmoja ambaye hata hivyo hakuweka jina lake hadharani.

Handeni Kwetu inawatakia waislamu wote Sikukuu njema ya Idd hapo kesho na kuwapa imani nzuri wengine wote duniani.

No comments:

Post a Comment