Pages

Pages

Thursday, August 08, 2013

Mapacha Watatu, Ally Nipishe kutambulisha nyimbo mpya Agosti 16


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu, inatarajia kutambulisha nyimbo zao sambamba na mwimbaji wa kizazi kipya, Ally Nipishe naye kutambulisha yake katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, Agosti 16 mwaka huu.
Vijana wa Mapacha Watatu pichani
Shoo hiyo ya aina yake itafanyika Ijumaa ya kwanza baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhan.

Maandalizi kabambe kwa ajili ya kuhakikisha kuwa bendi hiyo na kijana Nipishe wanafanya vizuri yanaendelea ili kuwapa raha mashabiki wao hapa nchini.

Nyimbo mpya za Mapacha Watatu inayojumuisha wakali kadhaa akiwamo Jose Mara na Khalid Chokoraa ni Kisu cha Kuokota, Furaha na Sauti ya Marehemu, wakati wimbo wa Nipishe unaitwa Nikupulike.

Mbali na nyimbo hizo, Mapacha pia wanatamba na nyimbo zao lukuki zinazopendwa na wengi katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment