Pages

Pages

Sunday, August 11, 2013

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF laipiga tafu ya Milioni 5.1 timu ya Boom FC


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa Boom FC umelishukuru Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kuipatia msaada wa Sh 5, 125, 000 kwa ajili ya uendeshaji wa timu hiyo katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa NSSF, Ramadhani Dau
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Boom FC, Duni Mibavu amesema fedha hizo zitasaidia timu kufanya vizuri katika ligi na kuwapa morali wachezaji ili kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

“Tunawashukuru wenzetu wa NSSF chini ya Mkurugenzi wake Dk. Ramadhan Dau kwa msaada mkubwa walioutupatia, hii inaonyesha ni jinsi gani walivyoguswa na na kilio chetu na kuamua kutusaidia ili tufanye vizuri,” alisema.

Duni ameomba na mashirika mengine pamoja na makampuni mbalimbali nayo kuiga mfano wa NSSF katika kuzisaidia timu za madaraja ya chini ili nazo zifanye vizuri.

No comments:

Post a Comment