Pages

Pages

Saturday, August 24, 2013

Msanii Recho wa THT awabeza wanaomsimanga



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI Winfirda Josephat, maarufu kama (Recho), amesema kwamba haoni sababu ya kupondwa na watu wasiopenda kufuata nyayo za mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila, Ray C.

Recho akiwajibika jukwaani
Waimbaji hao wawili wanafanana kwa sauti na aina ya uimbaji, jambo linaloleta mvutano kwa baadhi ya mashabiki wa muziki huo hapa nchini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Recho alisema kwamba ili msanii aweze kufika mbali lazima awe na mkongwe anayemfuata kisanaa.

Alisema kwake yeye Ray C ndio kila kitu kwake, hivyo haoni ubaya wa kufuata nyayo zake katika miondoko ya Bongo Fleva, ukizingatia kuwa hawezi kuharibu ndoto zao.

"Bado naweza kubaki kama Recho na yeye ataendelea kuwa Ray C, hivyo mashabiki wangu wana kila sababu ya kuniunga mkono ili nifikie malengo niliyojiwekea.

"Nitaendelea kuimba kwa kiwango cha juu ili niwe bora zaidi, bila kujali wale wanaofikiri sina sababu ya kuiga mazuri yanayofanywa na wakongwe ndani na nje ya nchi,” alisema Recho.

Mwimbaji huyo anatokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), yenye wakali kadhaa hapa nchini, akiwamo Barnabas, Amini, Mwasiti na wengineo.

No comments:

Post a Comment