Pages

Pages

Saturday, August 24, 2013

Maarufu ni wao na wabwia unga ni wao



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI Tanzania tu tunaoneana haya kuambiana ukweli, hasa hili sakata la kuona wasanii wengi wa nyumbani, wakiwamo wa muziki wa kizazi kipya wanavyotumbukia kwenye ubwiaji wa unga.
Msanii Diamond pichani.
Ni wavutaji wa dawa za kulevya. Tunaona jinsi hali zao kiafya au mwonekano wao katika jamii. Katika nchi za wenzetu, hasa nchini Marekani, kuambiana ukweli kwao ni jambo la lazima.
Ahmad Ally 'Madee'
Hapa kwetu mtu akiambiwa anakula unga, hata kama ikiwa kweli, atakataa au wale wanaomzuungaka, yani marafiki zao kumtetea, hivyo kumfanya aendelee na vitendo vyake.


Ney wa Mitego
Msanii Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C yeye alionekana shujaa mno alipoweka wazi. Hata hivyo si Ray C tu, ila wasanii wengi wao wanabwia unga.


Marehemu Albert Mangweha Ngwair, aliripotiwa kuzidiwa na dawa za kulevya zilizosababisha kifo chake.
Kwa mfano, kusikia au kuona mtu akisema hadharani Rihanna anakula unga au amefundishwa na swahiba wake Chris Brown ni rahisi mno, wakiamini kuwa jamii itajifunza.
Msanii Dayna pichani anapaswa ajichnge na dawa za kulevya
Unga unatajwa kuwa ni ulevi wa ghali ila kuanza kwake ni rahisi mno, huku kuacha kwake ikiwa kazi kubwa. Mtu anaweza kuanza kuvuta unga kwasababu mbalimbali.


Chipukizi wa Bongo Fleva, Vida naye anastahili kujichunguza na matumizi ya dawa za kulevya
Sababu hizo kubwa ni mtandao wa marafiki wanaotumia dawa za kulevya, hivyo mtu kuona kuna ulazima na yeye kuingia kwenye ulevi huo ili wafanane kitabia na mtazamo.
Lady Jay De, licha ya kuwa nyota wa muziki, ila anaweza kuathiri kipaji chake endapo atajiingiza kwenye matumizi hayo.
Tunaweza kuchukulia kiurahisi, ila suala la ulevi wa unga kwa wasanii wa Tanzania liahitaji nguvu za ziada na kuambiana ukweli. Wengi wao ni waathirika wa hilo.
Msanii Rehema Chalamila, Ray C ni mwathirika wa dawa za kulevya na wengine lukuki ambao bado wanafanya siri.
Wasanii kama vile Langa Kileo ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa kwenye ulevi huo. Ingawa mwenyewe mwanzo alikataa, lakini baadaye alikiri kula unga.


Profesa Jay mkali wa muziki wa Hip Hop Tanzania
Mwingine ni marehemu Albert Mangweha Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, akihusishwa kuzidiwa na dawa za kulevya. Ingawa ripoti yake ilivuja, lakini tulifanya kazi ya ziada kuuficha ukweli.
Mr Blue, alitamba sana wakati huo.
Hadi leo, hakuna aliyethubutu kuinua kinywa chake kuweka wazi kifo cha Ngwair, tukiamini kuwa tunamdhalilisha marehemu. Hii si kweli hata kidogo, maana woga wetu ndio chanzo cha kuhalalisha matumizi ya dawa za kulevya kwa jamii.
Linah, msanii kutoka THT
Kila mtu anajua jinsi matumizi hayo yanavyoharibu mfumo na mtazamo wa jamii, wakiwamo wasanii wanaotambulika kama kioo cha jamii. Katika kuliangalia hilo, nathubutu kusema kuwa katika kila wasanii 10, sita wanatumia dawa za kulevya.

Mara kwa mara tunaona jinsi baadhi yao wanavyoshindwa kufanya shoo zenye kuvutia mashabiki wao. Muda wote yupo nyuma ya jukwaa akivuta bange, unywaji wa pombe na kuchanganya na dawa.

Hilo ni jambo lenye kukera mno. Tuna hatari ya kupoteza wasanii wetu kutokana na matumizi hayo mabaya. Hii inahitaji kupeana elimu ya kutosha na kuambiana ukweli.
Tunaweza kumuona Ray C ni mtu wa ajabu mno, lakini kuna kundi kubwa la vijana wenzake katika Bongo Fleva wanaokula unga. Kesho tutaona aibu tutakapokosa nguvu kazi ya Taifa kwasababu ya kuathiriwa na matumizi hayo ya dawa za kulevya.

Kila mtu mwenye ukaribu na msanii wa Tanzania, lazima amwambie ukweli swahiba wake huyo, ndugu yake kuwa ulevi wa unga hauna thamani katika mwili na vipaji vyao.

Waache kwa ajili ya kujenga jamii bora. Ingawa ulevi huo unauzwa kwa bei ghari mno, lakini pia unasababisha mkanyanganyiko katika utendaji wa kazi kwa jamii na wasanii kwa ujumla.

Mlevi wa unga siku zote hapendi kusumbuka. Anapenda kukaa na kujidunga wakati wote. Hata kama ana akiba ya Milioni 50 katika akaunti yake, lakini kwakuwa ni anakula unga, hakika hizo zitakwisha kwa siku chache mno.

Wasanii hao ndio wale wanaoshindwa kabisa kufanya kazi zao kwa ufanisi, tena wengineo wakiwa wazito kabisa kupanda jukwaani. Msanii anajua kabisa kuwa ana shoo, lakini anapanda saa 9 usiku huku akiwa kwenye ulevi wa kupindukia.

Akipanda jukwaani hana anachoimba na kushuka. Kesho wasanii wenzake, mashabiki wake wanamuona mtu wa kawaida. Thamani yake inapotea na kuanza kuwashika uchawi wenzake.

Ndio maana nasema, wasanii wengi wanakula unga. Kulisema hili hatuhitaji kupata kibali cha Polisi, ukizingatia kuwa watu hao wanajulikana mwenendo wao kwa ujumla.

Tuwaambie ukweli, tuwakataze bila kuwaonea haya kwa ajili ya kujenga jamii bora, maana kila siku ya Mungu hali inazidi kuwa mbaya na kuwaweka wasanii mtegoni.

Dawa za kulevya ni tatizo kwa wasanii wetu.
+255 712 053949

No comments:

Post a Comment