Pages

Pages

Saturday, August 24, 2013

CUF yaanguka wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa Mkurugenzi wao kuhamia CCM


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Siasa na Uenezi wa wilaya Handeni mkoani Tanga wa Chama Cha Wananchi (CUF), Zuberi Mussa Abdulrahman, amesema hana haja ya kukaa kwenye chama kisichojitambua, ndio maana ameamua kurudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wafuasi wa CUF wakiwa kwenye mikutano ya chama chao.
Bosi huyo wa zamani wa CUF wilayani Handeni sasa yupo CCM baada ya kukiacha chama hicho kwa kipindi cha miezi miwili, huku akisema hakina mashiko na kimepoteza dira.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Mussa alisema CCM imekuwa ikifanya siasa safi na dhamira ya kuwaongoza Watanzania wote, hivyo kwake yeye kuhama CUF ni jambo la busara mno.

Alisema anaamini kwa sasa atashirikiana na viongozi wa CCM ili kufanikisha maendeleo ya Handeni na Tanzania kwa ujumla, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

“Siwezi kukaa kwenye chama ambacho sera yake haijulikani na kuchelewesha maendeleo ya Taifa kwa ujumla, ukizingatia kuwa kwa muda mrefu sasa CUF imekosa mashiko.

“Tangu nilipokihama rasmi miezi miwili iliyopita na kurudi CCM, maisha yangu yamekuwa na furaha kwa kuona wananchi wanashirikiana kwa kiasi kikubwa na serikali yao inayojali maisha yao,” alisema.

Kuhama kwa Mussa ni muendelezo mbaya wa maisha ya chama cha CUF wilayani Handeni mkoani Tanga, huku idadi kubwa ya viongozi wao wakiwa na lengo laa kukimbia na kuhamia kwenye vyama vingine vya siasa.

No comments:

Post a Comment