Pages

Pages

Sunday, August 18, 2013

Momba kumvaa Mwamakula leo Manzese jijini Dar es Salaam



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA Sadiki Momba amejigamba kumchakaza mpinzani wake Amos Mwamakula, katika pambano lao linalofanyika leo katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbwi hapa nchini, huku kila mmoja akiwa na imani ya kuondoka na ushindi dhidi ya mwenzake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Momba alisema kuwa amejiandaa vizuri kuhakikisha kuwa anaondoka na ushindi dhidi ya mpinzani wake.

“Nipo tayari kukabiliana na mpinzani wangu katika pambano ambalo nataka nishinde na kuwapa raha mashabiki wangu katika mchezo huo,” alisema.

Pambano hilo linafanyika likiwa ni la kuwania Ubingwa wa Taifa PST, ambapo linasubiriwa kwa hamu na wadau wa mchezo wa masumbwi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment