Pages

Pages

Sunday, August 18, 2013

Coastal Union kutia timu Moshi kujifua zaidi kwa ajili ya kivumbi cha Ligi Kuu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kitaondoka jijini Tanga Jumatatu ijayo kuelekea Moshi, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kukutana na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Binslum
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union yenye maskani yake mkoani Tanga, Nassor Binslum, alisema kuwa timu yao imeamua kuelekea Moshi kutokana na hali ya hewa ya mji huo kufanana na ya Arusha kama njia ya kuzoea hali ya baridi.

Alisema uongozi wao umeshauliana na Kocha Mkuu, Hemed Morocco ili timu yao watoke nje ya Mkoa wa Tanga ili waendelee na mazoezi yao kwa ajili ya kuwafanya watese katika patashika ya ligi ya Tanzania Bara msimu ujao unaoanza Agosti 24.

“Timu itaelekea Mombasa jumamosi hii kucheza mechi moja ya kirafiki, halafu itaelekea Moshi itakapoweka kambi mpaka tarehe 24 mwezi huu watakapoingia Arisha kucheza na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi,” alisema Binslum.

Kutokana na usajili wa mwaka huu wapenzi wengi wa soka Tanzania wamekuwa wakiitabiria kufanya vizuri Coastal Union kwani  timu nyingi zimeshindwa kutumia vema nafasi ya kusajili wacezaji wenye uwezo.

Coastal Union imefanikiwa kunasa wachezaji wawilai kutoka Simba SC, wawili kutoka JKT Oljoro, mmoja ktoka Jamhuri ya Pemba, mmoja kutoka Polisi Morogoro, mmoja kutok URA ya Uganda na mmoja kutoka Bandari ya Mombasa wakati mwingine ametoka Azam FC.

No comments:

Post a Comment