Pages

Pages

Sunday, August 18, 2013

Khalid Chokoraa: Sina ugomvi na Mwinjuma Muumini



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa dansi hapa nchini, Khalid Chokoraa, amesema kwamba anamuheshimu mwimbaji mwenzake Mwinjuma Muumini na hawana ugomvi kama inavyodaiwa na wadau wengine.
Mwinjuma Muumini akiimba jukwaani sambamba na Khalid Chokoraa

Hapo awali, wanamuziki hao walikuwa kwenye vita ya maneno wakisemana, ila juzi Chokoraa alitumia muda mwingi kumsifia Muumini na kusema kuwa wao ndi ndugu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chokoraa alisema kuwa anamuheshimu Muumini na hawana ugomvi, hivyo kilichokuwa kinasemwa ni mambo ya kawaida kwenye muziki.


Alisema ingawa walikuwa wakijibizana majukwaani, lakini ugomvi wao hauwezi kuendelea, hivyo wadau na mashabiki wa muziki wasitafsiri vibaya juu ya mkanganyiko huo.

“Namthamini kaka yangu Muumini kwasababu anajua kazi yake, ingawa hapo nyuma baadhi yao walijua labda nina ugomvi na ndugu yangu katika harakati za kimuziki,” alisema Chokoraa.

Chokoraa yupo kwenye bendi ya Mapacha Watatu, wakati Muumini yeye anaunda bendi ya Victoria Sound akiwa sambamba na Waziri Sonyo.

No comments:

Post a Comment