Pages

Pages

Saturday, August 03, 2013

Makamu wa Rais, Dkt Mohammed Gharib Bilal atoa neno katika hafla ya kukabidhi zawadi ya washindi wa kuhifadhi Qur'an Tukufu



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza za waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Waumini wa dini ya Kiislamu, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, katika Shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Waumini wa dini ya Kiislamu, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, katika Shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 2, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 30, Abdulkarim Khamis, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa  washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.

Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 1.5, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 20, Maryam Nassor (8), wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, kuzungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya Kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, wakati wa hafla ya kuwakirimu wasindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku Julai, 2, 2013. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment