Pages

Pages

Saturday, August 03, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU: Si wote wanaofurahia uhusiano wao



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI siku nyingine mimi na msomaji wangu tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi, ambapo tunachangia mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha.
Wapendanao pichani.
Nashukuru kwako wewe unayeguswa na safu hii na kuniunga mkono kila Jumamosi, nikiamini kuwa nitaendelea kuwapo hapa.

Ndugu msomaji wangu, kuna watu ambao katika uhusiano wao, kila siku wamekuwa wakiishi kwa malalamiko makubwa kiasi cha kuwaondolea hamu ya kubaki kwenye uhusiano wao.

Hawa ni wale wanapofikia muda wa kurudi majumbani mwao, hamu yote imekata. Wapo mabinti ambao wamekosa hamu kabisa ya kuingiliana kimwili na wapenzi wao, wakiwamo wale waliofanikiwa kufunga ndoa.

Kwa wale ambao bado ni wapenzi au wachumba, si tatizo, ila mbaya zaidi hali hii ipo pia kwa watu ambao wamefunga ndoa.

Utakuta mtu yupo na amani na furaha tele. Lakini anapofikiria kasumba ya kitandani, tumbo linamnyongolota.

Ukilifikiria suala hili, utadhani labda watu wa aina hiyo wanaumwa. Ila hapana, maana baadhi yao ni wavivu ama pia kuona ni uchafu.

Watu wanatofautiana, ndio maana linapoingia suala la aina hiyo, kitu kinachotwa ndoa hakiwezi kuwa na amani na kuwaridhisha wenzetu.

Kwa mfano, mwanaume aliyebahatika kuwa kwenye ndoa na mwanamke asiyependa kitendo cha haki ya ndoa, basi anaweza pia kushikwa na tamaa ya kujihusisha pia na watu wa nje.

Na sio mwanaume tu, ila hata mwanamke akiwa anaishi nwa mtu mvivu asiyejua namna gani ya kumridhisha mwenzake hawezi kufurahia ndoa.

Atakuwa na malalamiko tu. Ndio maana hata muda wa kurudi nyumbani unapofika, ataendelea kujizunguusha ili usiku uingie.

Hana cha kumuwahisha nyumbani, maana anajua hata akirudi nyumbani kwake usipoangalia anakuta kelele, au kutokupewa kile anachopenda.

Hii ni mbaya mno, hivyo kuna haja sasa ya kila mtu kujitafakari anavyoishi na mume au mke wake, kwa wale waliobahatika kufunga ndoa.

Sio kwa wana ndoa tu, hata wale waliokuwa kwenye upenzi wa kudumu na wenye muelekeo wa kuwa mwili mmoja, endapo uhusiano huo unahusisha tendo la ndoa basi ni wajibu kujiangalia vuzuri.

Nasema hivi huku nikijua kuwa Dunia ya leo, asilimia kubwa wanaofunga ndoa, basi lazima walikuwa kwenye uhusiano.
Si kama zamani mtu kufunga ndoa na msichana aliyemuona kwenye picha au aliyetafutiwa na ndugu zake kijijini nay eye kuletewa mke tu.

Leo vijana wanapenda kuonana kwanza ndio mambo mengine yafuate, ukiwa ni mpango wenye lengo la kuzoeana na kujuana tabia.

Huu ni wakati wa kila mwanajamii hasa wa Tanzania kuona namna gani anaweza kumfurahisha mtu wake ili kuepusha usaliti usiokuwa wa lazima.
Kama mtu anapewa kila anachohitaji kutoka kwa mume au mke wake, yakiwamo mapenzi ya dhati, sembuse wale wanaodhulumiwa haki ya ndoa?

Hii ni ngumu kuona penzi la kweli ndani yao. Kama wewe ni mmoja wa watu wasiowaridhisha watu wao katika ‘majambozi’, chunga sana.

Unaweza kuwa mlinzi wa nyumba bila sababu za msingi. Utalala peke yako muda wote, maana hujui makosa yako na hupendi kujifunza.

Jione mwenye makosa kwa mtu wako  na kutaka mabadiliko kuanzia sasa. Najua si kila mtu ni mjuzi katika masuala ya mapenzi, ila sioni kwanini usifanye yale yatakayompa raha na amani.

Ndugu msomaji wangu, kama wewe ni miongoni mwa watu, hasa wasichana ambao wanaona wanapata woga kujihusisha katika tendo la ndoa na watu wako, weka wazi kwa mawasiliano yetu hapo chini ili upate mbinu za kuweza kukomboa ndoa au uhusiano wako.

Na ndio maana tunaweka namba ya simu na barua pepe, ikiwa ni lengo la kuwekana sawa miongoni mwetu, maana si wote wanaofurahia uhusiano wao.

Ndio hao wanaojikunyata kitandani, wakiguswa tu wanakunja uso kama wamesikia harufu ya kinyesi, huku wakitetemeka kwa woga.
Jichunge na tukutane wiki ijayo.

+255 712 053949


No comments:

Post a Comment