Pages

Pages

Saturday, August 24, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU: Dalili ya anayejirudi kwa mpenzi wake wa zamani



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NAKUSHURU wewe unayeguswa na safu hii kiasi cha kuniunga mkono kila kila Jumamosi katika kujadili mambo yanayohusu mambo ya uhusiano na maisha katika jamii yetu.
Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nitashindwa kukushuru na kukutakia kheri pia wewe unayeona umuhimu wa kuipitia safu hii.

Ndugu msomaji wangu, katika uhusiano wa kimapenzi, kumekuwa na mapungufu mengi yanayoweza kutokea katika jamii yetu.

Hii ni pale mtu anaposhindwa kujizuia na mpenzi wake wa zamani kiasi cha kutia shaka. Hapo awali nilishawahi kuijadili suala hili.

Hata hivyo, suala hili ni pana mno. Wengi linawakabiri na kuwachanganya kisaikolojia. Kuna mengi yanaweza kutokea ndani yake, ila hii ni dalili ya wazi kuwa mtu wako anaendelea kumpenda aliyeachana naye.

Kuna watu ambao licha ya kuachana na wapenzi wao wa zamani, lakini bado hawawezi kuwa mbali nao kwa kiasi kikubwa.

Kwa mfano, kuna mtu ambaye muda mwingi anakesha katika albamu akimuangalia mpenzi wake huyo aliyeachana naye.

Kama sio albamu, pia ni ngumu kumshauri azitupe au kuzirejesha nguo zilizokuwa zinatumiwa na mpenzi wake wa zamani ili kuondoa usumbufu.

Kuna msomaji wangu mmoja ameonyesha kuumizwa kichwa na suala hili. Huyu alisema kuwa ana mpenzi wake, ila anamshangaa anapozihifadhi nguo na vitu vyote vilivyokuwa vinatumiwa na mtu wake.

Mbaya zaidi, alipoamua kuzichoma baadhi yake, aliingia kwenye kadhia ya kutukanwa na mtu huyo. Hili ni jambo la kushangaza mno.

Wewe kama umeachana na mtu wako, unawezaje kuhifadhi vitu vinavyoweza kukumbusha matukio ya nyuma?

Kwanini uishi kwa kumsumbua mwenzako hadi ashindwe kulala usingizi kwa sababu yako binafsi? Ni wazi mtu yoyote mwenye mtazamo huu, basi ni ishara kuwa hawajaachana.

Hata kama ameachana naye, basi si chache zijazo atarudiana naye. Wewe uliyekuwa kwenye uhusiano wa aina hiyo lazima uwe makini.

Nasema hivyo kwasababu kama upon a mtu ambaye muda mwingi anashindwa kumsahau mpenzi wake wa zamani, ni wazi kuwa uwapo una mashaka.

Huenda ameshindwa kabisa kutulia kutokana na nafasi yako, hivyo ni wakati wako kuumiza kichwa kwa ajili ya kujua cha kufanya.

Inawezekana kabisa ukawa kwenye hisia na mpenzi wako wa zamani, ila kwakuwa umeshaachana naye kwanini ushindwe kumsahau?

Ili tuweze kufurahia mapenzi, lazima tuwe makini katika mambo yetu. Hakuna haja ya kujiingiza katika uhusiano ambao una mashaka.

Kwa wewe uliyekuwa kwenye uhusiano wa aina hiyo, unapaswa ujiangalie ili usiingie kwenye wasiwasi wa kujipotezea muda wako.

Hakuna haja ya kuishi kwa wasiwasi kwasababu ya mtu ambaye anashindwa kabisa kujisahaulisha ili aweze kutumia muda huo kulipa fadhira ya upendo wako.

Ni wakati wako kujua kuwa kama upo kwenye uhusiano na mtu ambaye chumbani kwake amehifadhi nguo au vitu vingine vya mtu wake wa zamani kuwa bado anamuwaza na hawezi kumsahau.

Mbaya zaidi pale unapomshauri mazuri yeye akakuona huna lolote la kumwambia kwa ajili ya maisha ya upendo wenu kwa ujumla.

Hayo ni mapenzi yenye kuumiza kichwa. Kama mtu anashindwa kumsahau mtu wake huyo, basi wakati wowote mapenzi yao yataanza upya.

Ndio hao licha ya kuachana na mtu, lakini muda mrefu wapo katika mawasiliano kiasi cha kuibua maswali lukuki kutoka kwenye jamii.

Huo ndio ukweli wa mambo, hivyo lazima kila mmoja wetu awe makini kama ana lengo la kujipa furaha katika moyo wake, vinginevyo ni maumivu.
Tukutane wiki ijayo.
+255 712053949
 

No comments:

Post a Comment