Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

Kupigwa risasi kwa Sheikhe Ponda Watanzania wavutana, kila mmoja akisema lake, vyombo vya habari vya Kimataifa vyamuhusisha na kumwagiwa tindikali mabinti wa Uingereza



Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa amelazwa katika chumba maalum katika Kitengo cha Mifupa Moi, jijini Dar es Salaam, wakati akisubiri kufanyiwa operesheni katika bega lake la mkono wa kulia baada ya kupatwa na jeraha linalodaiwa kuwa limetokana na kupigwa risasi na Polisi mjini Morogoro hivi karibuni.


MVUTANO mkubwa umeendelea kuibuka baada ya Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu Tanzania, Sheikhe Issa Ponda, kudaiwa kupigwa risasi mkoani Morogoro kwenye kongamano la Idd El Fitr mwishoni mwa wiki iliyopita.

Watu mbalimbali kwenye jamii wamekuwa wakivutana kuelezea kadri wanavyojua wao namna gani unyama aliofanyiwa Ponda, huku baadhi yao wakisema amejitakia kwasababu ya kuleta uchochezi.

Hata hivyo, BAKWATA wao ambao ndio mahasimu wakubwa na Ponda, wamejitokeza jana na kuelezea kuumizwa na kitendo alichofanyiwa Ponda, ikisemwa hakijafanywa na binadamu wa kawaida.

Kwa sasa Ponda yupo Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu yake, baada ya kupelekwa usiku wa manane akitokea mkoani Morogoro.

Katika hatua nyingine, vyombo vya habari vya Kimataifa, yakiwamo magazeti ya nchini Uingereza yamekuwa yakimuhusisha Ponda moja kwa moja kwenye tukio la kumwagiwa tindikali kwa matinti wa Uingereza Kirstie Trup na mwenzake Katie Gee mjini Zanzibar.




No comments:

Post a Comment