Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

Coastal Union wana usongo na Ligi Kuu ili wawape raha Wagosi wa Kaya mkoani Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga, umesema umejipanga imara kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika patashika ya Ligi ya Tanzania Bara, itakayoanza Agosti 24 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Bin Slum, akiwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Coastal inaendelea na mazoezi makali ya kujiweka fiti kwa ajili ya kuifanya timu yao ilete ushindani katika msimu huu, sambamba na kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Yanga.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora, alisema kuwa vijana wao wanafanya mazoezi makali, pamoja na kucheza mechi nyingi za kirafiki.

“Tunaingia uwanjani kucheza mechi za kirafiki mara kwa mara, tukiamini kuwa ni sehemu ya maandalizi yetu kwa ajili ya ligi,” alisema Aurora.

“Tunaamini kuwa mambo yetu yatakuwa mazuri kwa ajili ya kulinyakua taji la Ligi, ambapo mipango ni kuhakikisha kuwa sisi tunafanya vyema, hivyo tunaamini suala hili litafanikiwa kutokana na mipango,” alisema.

Ili kuboresha kikosi chao, Coastal iliwaongeza wachezaji kadhaa akiwamo Haruna Moshi Boban na Juma Nyoso, moja ya wachezaji wenye uwezo na majina ya kutosha katika ligi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment