Pages

Pages

Monday, August 12, 2013

Wizara ya Maliasili na Utalii watolea ufafanuzi sakata la ufisadi wizarani hapo



 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MALIASILI NA UTALITAARIFA KWA UMMAWIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEKANUSHA UVUMI KUWAWATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI

Wizara ya Maliasili na Utalii inakanusha uvumi ulioandikwa
Na kuchapishwa na gazeti la Raia Mwema namo tarehe 07/08/2013 ukurasa wa kwanza lililobebakichwa cha habari UFISADI kama wabunge, wateule wa waziri wasaini poshomara mbili ikiwa na ufafanuzi kuwa yumo Ofisa Takukuru,walipwa na taaasisiwanayoichunguza.

Taarifa hii ilikuwa na muendelezo zaidi ukurasa wa tatu wagazeti hilo.Wizara inasisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:

Wajumbe wa kamati husika (iliyoundwa kuchunguza tuhuma kuhusumatumizi mabaya ya fedha unaowahusisha watendaji wa Mamlaka yaHifadhi ya Ngorongoro) (NCAA) HAWAKULIPWA POSHO MARAMBILI.

Malipo waliyolipwa wajumbe wa kamati husika yalilipwa na Mamlaka yaHifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kama ilivyo kwenye Hadidu za Rejea zakazi husika na hawakulipwa malipo yoyote na wizara ya maliasili na utalii.

Viwango vya posho vilivyotumika ni kwa mujibu wa Waraka wa Serikalinamba 2 wa Mwaka 2010, Ref.Na C/AC/.17/45/01/125

Malipo yaliyofanywa kwa wajumbe wa kamati husika yalikuwa na kibalihalali cha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Suedi Kagasheki

Kamati husika ilifanya kazi vizuri na kukabidhi ripoti ya awaliiliyomridhisha Waziri Kagasheki aliyewaagiza kuifanya kazi tajwa hapo juu.Ripoti hiyo ya awali na hii ya mwisho ZITAWEKWA HADHARANI iliUmma uelewe hali halisi ya Mamlaka ya Ngorongoro na siyo upotoshaji waRaia Mwema.

Kamati iliyoundwa na Waziri Kagasheki ilikuwa na kazi tofauti na ilekamati ya awali iliyowahi kuongozwa na Jaji Robert Mihayo aliyeteuliwa naaliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige mwaka 2011.

RaiaMwema ingejiridhisha kwa kutazama hadudi za rejea za Kamati hizo mbili.Si jambo jema Raia Mwema kuupotosha Umma.Wizara ya Maliasili na Utalii imesikitishwa na kitendo cha gazeti la Raia Mwema,gazeti ambalo limejijengea sifa na kuaminiwa na jamii kwa kutoa taarifa zauhakika zinazofuata maadili ya utoaji taarifa kwa vyombo vya habari, kuchapishahabari zinazochafua jina la Wizara, Wabunge na Serikali kiujumla bilakujihakikishia ukweli wa taarifa hizo kutoka wizara husika.

Kwa taarifa hii, Wizara inalitaka Gazeti la Raia Mwema kufuta uvumiwaliochapisha kwenye gazeti lao kama ilivyotajwa hapo juu na pia kuiomba radhiWizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchapisha habari ambazo si sahihi na pia
 
kuchafua jina la Wizara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALIWIZARA YA MALIASILI NA UTALII 12/08/2013

No comments:

Post a Comment