Pages

Pages

Friday, August 30, 2013

Diamond sukari ya warembo afanya kufuru, amnunulia gari mzee Muhidin Gurumo sambamba na kutambulisha video mpya ya My Number One


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII Nassib Abdulmalick maarufu kama Diamond Platinum, ameonyesha yeye ni mkali na mwenye fedha nyingi baada ya kukusanya watu kibao katika hoteli ya Serena, Posta, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa video yake ya My Number One.
Msanii Diamond akiwa Serena Hoteli alipozindua video ya wimbo wake wa My Number One.
Mbali na uzinduzi huo, pia msanii alitumia fursa hiyo kumkabidhi gari alilomnunulia mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Gurumo, aliyestaafu muziki, huku akisema hajafanikiwa kununua hata baiskeli.


Diamond akimkabidhi mzee Muhidin Gurumo gari, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kustaafu muziki.
Katika mazungumzo yake, Diamond alisema kuwa anathamini mchango wa wanamuziki waliyotangulia, kwakuwa wao ndio waliyosababisha sanaa yao izidi kuchanja mbuga.


"Namthamini mno mzee Gurumo na wanamuziki wengine wote wa Tanzania, maana bila wao sisi tusingeweza kusimama hapa tulipokuwa sasa, ukizingatia kuwa wao ndio kila kitu," alisema Diamond.

Naye mzee Gurumo alisema haamini macho yake baada ya kupewa ufunguo wa gari lililonunuliwa na msanii Diamond, ambaye kwake ndio chaguo kwa waimbaji wa Bongo Fleva,.

"Namshukuru huyu kijana na Mungu ampe mafanikio makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya ili aendelee kuwa juu zaidi kwa kitendo chake hiki ambacho kinashangaza wengi," alisema.

Diamond ndio msanii wa kwanza kufanya kitendo cha kiungwana kama hicho, huku pia mkutano wake ukifana kwa kualika wadau mbalimbali wenye majina yao kwa ajili ya kushuhudia anachofanya ndani ya Hoteli ya Nyota tano ya Serena, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment