Pages

Pages

Thursday, August 29, 2013

Diamond kuonyesha Ubillionea wake kwa kuwaita waandishi kwenye hoteli ya nyota tano


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LEO usiku msanii wa Tanzania, Nassib Abdulmalick maarufu kama (Diamond), anaonyesha utajiri wake, baada ya kuwaita waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, likiwa ni tukio la kihistoria kuwahi kufanywa na msanii wa Bongo Fleva, ukizingatia kuwa mpango huo unafanywa zaidi na wakali wa Kimataifa, hususan nchini Marekani wanapokanyaga ardhi ya Bongo na kuondoka.
 Msanii huyo anakutana na waandishi wa habari za burudani, ikiwa ni siku chache baada ya uvumi mkubwa kuenea kuwa naye ametajwa katika risti ya wanaosafirisha dawa za kulevya.
Msanii Diamond akiwa na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu. Picha hii ni kabla ya wawili hao kuachana. Hata hivyo Diamond amekuwa akisisitiza kuwa Wema ana mchango mkubwa katika mafanikio yake kimuziki.

Diamond aliyeibuliwa na wimbo wake 'Kamwambie', amekuwa nyota na mvuto wa aina yake, huku kila wimbo anaotoa ukiwa moto wa kuotea mbali na kushangaza namna ya kipaji chake.

Mapema wiki iliyopita Diamond aliwaambia Watanzania kuwa umaarufu wake na mafanikio yametokana na mikakati pamoja na kufanya kazi kubwa kutangaza kipaji chake.

“Nimefanya kazi kubwa sana ili nijiweke katika kilele cha mafanikio, hivyo naoma watu wasifikiri mengine yasiyokuwa na maana, ukizingatia kuwa nilipotoka huko najua mimi.

“Nimevumilia mengi yenye kusikitisha, hivyo chochote ninachokipata kwa sasa ni faida ya kujituma kwangu na si vinginevyo,” alisema Diamond.

Pamoja na yote hayo, wachambuzi wa mambo ya sanaa na muziki wa Bongo Fleva wanaamini kuwa Diamond umaarufu wake umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mwanadada Wema Sepetu, jambo ambalo hata yeye mwenyewe alikiri kwa Watanzania wote namna gani anathamini na kutambua uwapo wa mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake.

Ni kutokana na hilo, Diamond leo anautangazia umma kuwa yeye ni mkali na mwenye mafanikio makubwa kisanaa baada ya kudhamiria kuzungumza maisha yake ndani ya hotel yenye hadhi ya aina yake, ambapo pia atatumia muda huo kutambulisha video yake mpya.

No comments:

Post a Comment