Pages

Pages

Saturday, August 24, 2013

Mdogo wake marehemu Kanumba aibuka jijini Dar es Salaam na kutoa maneno mazito, amlillia kaka yake, apata msoto kulilia sanaa ya Tanzania



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MDOGO wake marehemu Steven Charles Kanumba, anayeitwa Lameck Charles Kanumba, ameibukia jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa kaka yake anamtokea ndotoni na kuzungumza naye mambo mengi, yanayohusu familia na sanaa ya Tanzania.
Lameck Charles Kanumba anavyoonekana kwa karibu, baada ya kuzungumza mengi na Handeni Kwetu Blog.
Lameck aliyasema hayo mapema leo mchana, ikiwa ni miezi mine tangu alipokuja jijini Dar es Salaam kwenye kumbukumbu ya kaka yake, ambapo pia historia inafanana kutokana na baba yao kuendelea kula kona na kuacha kuwatunza watoto wake na kuwatelekeza kwa mama zao.


Charles mdogo wake Kanumba anavyoonekana pichani
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Lameck alisema kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam, ambapo pia anatumia nafasi hiyo kuhangaikia masuala ya sanaa ambayo yapo kwenye damu yake.
Marehemu Steven Kanumba.
Alisema hawajawahi kuonana uso uso kwa Kanumba, kutokana na yeye kuishi mkoani Mbeya na mama yake, wakati siku anakufa alishindwa kupata nauli ya kuja kwenye mazishi yake.
“Naendelea kuumia kutokana na kufariki kwa kaka kabla ya kuzungumza naye uso kwa uso, lakini pia inashangaza kwakuwa mara kadhaa huwa ananijia ndotoni na kuzungumza naye hasa mambo yanayohusu familia.

“Baba hajanihudumia tangu mtoto kama ilivyokuwa kwa kaka Kanumba, hivyo bado naona nina mengi ya kufanya kwa ajili ya kumuenzi marehemu aliyeifanyia mambo mema Tanzania kwa kupitia sanaa,” alisema.

Aidha, Lameck yupo katika maandalizi kabambe ya kuandaa filamu yake inayojulikana kwa jina la ‘Charles’, huku akiishi kwa msamaria mwema, anayelikana kwa jina la Fatuma au mama Kenge, mtaa wa Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment