Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

Mabondia wataka kuzichapa kavu kavu

Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao.
Simba Watunduru.

Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam. Picha na Super D.

Na Super D, Dar es Salaam
 MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wamekiuka miko ya mchezo wa masumbwi baada ya kuchapana makonde kavu kavu mbele ya Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa utiaji saini mkataba  wa makubaliano wa kupambana mchezo wa kirafiki August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee

Akizungumzia tukio hilo rais huyo alisema sijawai kuona vitu kama hivi vya ajabu mana vijana wamekamiana mpaka kufikia atua ya kuchapana kavu kavu mbele yangu ata hivyo mzozo uwo umekubaliana kumalizika siku ya mpambano wao  ambapo atajulikana nani mbabe zidi ya mwenzake

Nae bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo uho ameaidi kumaliza mapema mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia Simba ame aidi kumchapa class kwa K,O

wakati wowote ule unajua huyo ni kijana mdogo sana mmemuaisha kwangu sasa siku hiyo mimi nita mpiga K,O mbaya sana najua kuwa  kwa Tanzania hii mimi ndie naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa K,O pindi nikutanapo uringoni
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'.

 
 

No comments:

Post a Comment