Pages

Pages

Sunday, August 18, 2013

Cheza Kidansi lafana Vijana Social Hall Kinondoni kwa kuwezeshwa na mchumi wa CCM Makumbusho, Yusuphed Mhandeni



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAMASHA linalojulikana kama Cheza Kidansi (CK) lililofanyika juzi katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni na kudhaminiwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mchumi wa Kata ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam, Yusuphed Mhandeni, lilikuwa la aina yake kwa kuhudhuriwa na watu wengi, bila kusahau bendi tatu kubwa kufanya shoo ya aina yake.
Vijana wa Diamond Sound Original wakiwajibika jukwaani.
Cheza Kidansi lilimualika Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, huku bendi zilizotumbuiza katika tukio hilo la kusherehekea mwaka mmoja ni Victoria Sound, Mapacha Watatu na Diamond Sound Original.

Akizungumza katika burudani hizo zilizokuwa na lengo la kuhamasisha na kukuza muziki a dansi Tanzania, Mhandeni alisema kwamba lengo lao ni kuona muziki unarudi juu kwa kasi kama ilivyokuwa awali.

Alisema muziki wa dansi una historia kubwa kwa Taifa la Tanzania, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa dansi inarudi juu naa kufanya vyema katika tasnia ya muziki huo.

“Nimehamasika sana na muunganiko huu wa vijana wa Cheza Kidansi walioanzia katika mitandao ya kijamii face book na baadaye kuona wakutane ili wajuane na kuzungumza jambo moja la muziki wa dansi.

“Nashukuru kwa kila mmoja wake kuhamasika pamoja na bendi zote zilizokubali kuja kujumuika na vijana hawa, ukizingatia kuwa ndio sababu ya kuwapo katika tukio hili la aina yake,” alisema Mhandeni.

 Naye Mnyonge alisema ni wajibu wa kila mmoja wao, wakiwamo viongozi wa serikali kuzialika bendi katika matukio yao ili kuwaongezea kipato, badala ya kuelemea kwenye muziki wa kizazi kipya.

Mbali na kuwa mdhamini wa tukio hilo la Cheza Kidansi, Mhandeni pia ndio mlezi wa muunganiko huo wenye lengo la kutafuta nguvu ya kuurudisha juu muziki wa dansi unaolekea kushuka siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment