Pages

Pages

Monday, August 19, 2013

Asha Baraka awaacha hoi watu kwa kumkimbia Mwinjuma Muumini ili asimuimbe jukwaani



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, juzi aliwaacha watu hoi baada ya kumkimbia Mwinjuma Muumini kwa madai kuwa anaweza kumuimba jukwaani.
Asha Baraka kulia akiwa na Deo Mutta Mwanatanga
Kali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, baada ya wawili hao kukutana kwenye matukio ya kimuziki wa dansi hapa nchini na kuhudhuliwa pia na wadau mbalimbali.
Mwinjuma Muumini, akiwa jukwaani.
Mara baada ya MC kumuita Muumini na bendi yake ya Victoria Sound jukwaani, Asha alinyanyuka kitini na kubeba kilichokuwa chake na kutoka zake nje.

Jamani acheni niondoke, maana naogopa kuimbwa na Muumini pale jukwaani,” alisema Asha kwa wadau wachache, akiwamo Engi Muro Mwanamachame na Abdulfareed Hussein.

Wimbo anaogopa Asha ni ule unaojulikana kama ‘Shamba la Bibi lina Magugu’ unaodaiwa kuwa ameimbiwa mwanamama huyo kutokana na bendi yake ya Twanga Pepeta kuwa na wimbo wa ‘Shamba la Twanga’.

No comments:

Post a Comment