Pages

Pages

Monday, August 19, 2013

Victoria Sound yamvua ubosi Mwinjuma Muumini na kumpa madaraka Kassim Muhumba

KIMENUKA. Uongozi wa bendi ya Victoria Sound umemuondoa katika nafasi ya urais Mwinjuma Muumini na kuzua hofu katika mustakabali wa bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka jana.
Mwinjuma Muumini, akiwa jukwaani
Nafasi ya Muumini kwa sasa inashikiliwa na Kassim Muhumba, huku Kocha wa Dunia akibaki kama mwanamuziki wa kawaida. Mabadiliko hayo yamekuja siku moja baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa kumekuwa na msigano wa aina yake katika bendi hiyo, huku yakifanywa na mmiliki wa bendi hiyo Daniel Denga, alipozungumza na waandishi wa habari.

Kocha wa Dunia alitangaza hali ya hatari asubuhi ya leo akielezea msigano uliokuwapo ndani ya Victoria Sound, yakiwamo mambo ya kutosikilizana ndani, jambo linaloonyesha kuwa ni ngumu bendi hiyo kuwa kileleni kama purukushani hizo zitaendelea.

No comments:

Post a Comment