Pages

Pages

Tuesday, July 09, 2013

Yanga kuendelea kula bata mkoani Tabora leo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga, leo itaaondoka mkoani Shinyanga na kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya kuendeleaa na ziara yao na kuwatembelea wadau na mashabiki wao mkoani humo.

Wakiwa huko, timu ya Yanga itaendelea na mazoezi yake sambamba na kucheza mechi za kirafiki na timu kadhaa mkoani Tabora.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Akizungumza jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa baada ya kutoka mkoani Mwanza na kutua Shinyanga, wameona waelekee Tabora kabla ya kupanga safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Alisema ziara hiyo ni sehemu ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara, wakiamini kuwa pia utakuwa utaratibu mzuri wa kurudisha fadhira kwa mashabiki wao.

“Bado tutaendelea kuwa mikoani, maana kesho (leo) msafara wetu utaelekea mkoani Tabora ambapo huko tutacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo bado hatujaijua.

“Ziara hii ipo kwa ajili ya kuwatembelea mashabiki wetu kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora, ikiwa ni kawaida kwetu Yanga,” alisema.

Ligi ya Tanzania Bara ambapo Yanga ndio bingwa mtetezi wake inatarajia kuanza kutimua vumbi mwezi ujao, huku timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo zikiendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa patashika hiyo.

No comments:

Post a Comment