Pages

Pages

Tuesday, July 09, 2013

Misri kwazidi kuchafuka na kusababisha vifo vya watu wanaopinga Rais Morsi kupinduliwa nchini humo




Hali ya amani nchini Misri imeingia katika wasiwasi mkubwa, huku ripoti zikionyesha zaidi ya wananchi 42 wamefariki Dunia kutokana wafuasi wa Rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, Mohammed Morsi kuandamana kushinikiza kiongozi wao arudishwe madarakani.

Picha zinaonyesha jinsi wananchi hao baadhi yao walivyofariki Dunia kutokana na machafuko hayo nchini Misri, tangu mapinduzi hayo yalivyobarikiwa na Jeshi la nchi hiyo.
 


Tunataka haki ya Rais Morsi.



Maafisa wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika, huku mamia mengine ya watu yakijeruhiwa katika kadhia hizo ikiwa ni harakati za kutafuta haki kama wenyewe wanavyosikika wakipaza sauti zao juu za kumlinda kiongozi wao huyo.

Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia, huku likilaumu jeshi kwa kuwaua raia wake na kutolea mfano wa Mkuu wa Jeshi Abdel Fattah Al-Sisi kama muuaji Mkuu na kusema yeye ndio kinara mkuu na anayejaribu kuondosha uhai wa watu wa Misri wanaolilia haki, tangu rais huyo aliyechaguliwa kihalali apinduliwe.


Haya ndio matokeo ya kisiasa nchini Misri na kuzua taharuki kubwa tangu tangu mapinduzi hayo yalivyofanyika na kusababisha kutoelewana kwa pande tofauti.

No comments:

Post a Comment