Pages

Pages

Tuesday, July 09, 2013

Treni ya Mwakyembe yabuma tena, yasimamisha safari zake kwa siku mbili jijini Dar es Salaam

UONGOZI wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL, umesema kuwa wananchi na wakazi wa jiji kwa jumla kuwa huduma ya treni ya jiji haitokuwepo kwa muda wa siku 2 kuanzia jana Julai 8 hadi leo, ambapo huduma hiyo itaanza kupatikana tena kesho.

Taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Afisa Uhusiano wa TRL kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Aman Kisamfu, ilisema kuwa uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi unaosimamia uendeshaji wa huduma hiyo jijini, huku ukisema kuwa utaratibu wa huduma hii huendeshwa kwa kutumia vichwa vya treni vitatu ambapo viwili uhudumia moja kwa moja na cha tatu huwa cha akiba.

Kuanzia siku ya Jumamosi ambapo huduma haikuwepo, kichwa cha tatu kiligundulika kuhitaji matengenezo makubwa na kupelekwa katika karakana yetu ya Morogoro.

Kutokana na utaratibu tulioainisha hapo awali kukosekana kichwa cha dharura ’standby’ kunalazimisha tusitishe huduma kwa muda. Hata hivyo Wahandisi na Mafundi wa Karakana yetu Kuu Morogoro wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla ya siku ya Jumatano na hivyo kutoa fursa huduma hiyo kuanza tena siku ya Jumatano Julai 10, 2013.

Uongozi wa TRL unawaomba radhi wakazi wa Jiji na kuwataka kuwa na uvumilivu wakati huu wa ukarabati kichwa cha treni unaoendelea na kwamba muda sio mrefu Wanareli wa TRL watafanya kila linalowezekana kuirejesha huduma hii walioizoeya.


No comments:

Post a Comment