Pages

Pages

Saturday, July 13, 2013

Wizara ya Maliasili na Utalii wafurahia mafanikio ya maonyesho ya Sabasaba



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imewashukuru watu wote waliotembelea wizara yao katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salam na  kuwawezesha kuibuka mshindi wa Kwanza wa Banda Bora katika kundi la Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya 37 ya Saba Saba 2013.
Ushindi mtamu ehe. Ndivyo wanavyofurahia wadau hawa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Ushindi huu unaama kubwa sana kwetu kwani haikuwa rahisi kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiingia kwa wengi bandani kwetu wanapata elimu yakutosha kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale waliokuwa wakitoa elimu mbalimbali zikiwemo za uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ufugaji nyuki na utalii.


Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakijiachia katika maonyesho ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotumwa Handeni Kwetu na Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Tulizo Kilaga, ilisema kuwa mwitikio huo umewafanya wajione ni washindi katika maonyesho hayo ya kibiashara.

“Aidha wale ambao hawakujaaliwa kwa sababu moja ama nyingine kufika kwenye banda letu  wasiwe na wasiwasi wanaweza kuungana nasi kwenye Maonyesho ya Nanenane Dodoma ambapo tutahakikisha tunafanya vema zaidi. 

“Sambamba na hilo Wizara inachukua fursa hii kuomba radhi kwa wale wote wailiokwaza kwa namna yoyote ile katika kipindi chote cha Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 37 kwani tunatambua wananchi wengi mlikuwa na kiu ya kutembelea banda la wanyama hai hata muda ambao tulilazimika kulifunga (saa kumi na mbili jioni) kutoa fursa kwa wanyama kupumzika na kupata mlo wao wa usiku,” ilisema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment