Pages

Pages

Friday, July 12, 2013

Mwanamuziki wa Extra Bongo akatwa sikio na vibaka, wakitaka kumpora



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MPIGA Tumba wa bendi ya Extra Bongo, Next Level, ama wazee wa Kizigo, Salum Chakuku, amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na vibaka na kuambulia kukatwa sikio lake la kushoto.

Mpiga Tumba wa Extra Bongo, Salum Chakuku, akionyesha jeraha lake baada ya kukatwa sikio na vibaka.

Taarifa za kuvamiwa kwa mwanamuziki huyo zimefika Polisi na kupewa  jalada KON/RB/1038/2013, ambapo tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita Mbagala Mzinga, jijini Dar es Salaam, wakati anarudi kutoka kwenye majukumu yake ya kila siku.

Mpiga Tumba huyo alidaiwa kuwa wakati anarudi kutoka kwenye shoo ya bendi yake ya Extra Bongo, ndipo alipokutana na vibaka hao na kumvamia ili wamzuru na kufanikiwa kukata sikio lake.

Habari hizo zinaeleza kuwa kabla ya kuvamiwa na vibaka, Chakuku alipelekwa nyumbani kwao na Mkurugenzi wake Ally Choki, walipotokea kwenye shoo yao ya Meeda inayofanyika kila Jumamosi.

Chakuku alisema kuwa alifanikiwa kupambana na vibaka hao ili wasimzuru zaidi, ambapo alijikuta akikatwa sikio lake la kushoto na kuwahishwa Hospitalini, ambapo vibaka hao walikuwa na silaha mbalimbali, yakiwamo mapanga na visu kwa ajili ya kufanikisha uhalifu wao.

No comments:

Post a Comment