Pages

Pages

Saturday, July 13, 2013

Coastal Union yapenya nusu fainali mashindano ya Rolling Stone jijini Arusha



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ndogo ya vijana ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kupenya nusu fainali ya mashindano ya Rolling Stone yanayofanyika jijini Arusha.
Kikosi cha leo kilichoanza Robo fainal dhidi ya Dareda fc asubuhi Hii. 1 Mansoor Alawi 2 Hamad Juma 'Basmat' 3 Mwaita Swalehe 4 Yusuph Chuma 'Croach' 5 Nzara Ndaro 'Nahodha' 6 Hussein Amir 'zola' 7 Muhammed Issa 'Banka' 8 Behewa Sembwana 9 Muhammed Hassan 10 Ali Nassor 'Ufudu' 11 Ayubu Semtawa.



Coastal imetinga nusu fainali baada ya kuwafunga bao 1-0 timu ya Dereda, lililowekwa kimiani na Ayubu Semtawa dakika ya 64 na kufanikiwa kupenya hatua hiyo muhimu na kuwapa raha mashabiki wao wa soka, hususan wa mkoani Tanga.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Meneja wa Coastal Union, Abdulrahman Ubinde, alisema wanashukuru kwa vijana wao kufanya vizuri katika mashindano hayo na kutinga nusu fainali.

Alisema kuwa wanaamini wataendelea kujiweka sawa katika kuiandaa timu hiyo ya vijana ili waendelee kufanyaa vyema katika mashindano hayo ya vijana yenye umuhimu mkubwa.

“Tunashukuru kwa vijana wetu kuendelea kuwapa raha wadau wa soka wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, baada ya kupania kurudia historia ya mwaka jana walipotinga fainali nchini Burundi.

“Lengo ni kutinga fainali kwa ajili ya kunyakua Kombe hilo ambalo kwa mwaka huu linafanyika hapa jijini Arusha, hivyo tutaendelea na harakati zetu na kuwapaa moyo wachezaji wetu,” alisema Ubinde.

Timu ya Coastal Union ni miongoni mwa klabu zilizoweka mikakati kabambe ya kuwekeza katika soka la vijana, jambo linaloleta picha nzuri ya kukuza soka hapa nchini.


No comments:

Post a Comment