Pages

Pages

Saturday, July 27, 2013

Wasanii wetu acheni vituko mitaani, tumechoka



Je, mzima?
NATUMIA muda huu kuwakumbusha wasanii wetu juu ya kuacha vituko vyao mitaani, maana wao ndio vinara wakati wanajua kuwa usanii ni kioo cha jamii.
Msanii Aunt Ezekiel akijiachia kama unavyomuona hapo.
Kwa kufanya hivyo, jamii itanufaika kutoka kwao, jambo ambalo kwa sasa ni gumu kulipata kutoka kwa wasanii wetu wanaoishi kwa vituko na kuandikwa vibaya magazetini.

Nasema hivi kwasababu mimi ni shabiki wa sanaa na wasanii, hivyo inapotokea mapungufu kama haya ya kutia hawanazo siwezi kubaki kimya nikililia maendeleo ya kazi yao.

Ni kwasababu hiyo, naomba wasanii wetu waone yale yenye kutia moyo na kuelimisha jamii, huku vitendo vya kufanya uhuni, uvutaji wa dawa za kulevya, uzinzi na uchafu mwingineo wauache.

Naamini kwa kufanya hayo, sisi wadau wao tutanufaika kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kuwa msanii anapofanya lolote, kuna wanaopenda kuwaiga kwa sababu za aina mbalimbali.

Kwa mfano, leo msanii hata akivaa nusu uchi, akapita mtaani kwao, basi wale wanaowaona nao wanatamani kuwa kama hao, hivyo kuonyesha hasara kubwa katika jamii yao.

Jambo hili haliwezi kukubalika hata kidogo, ndio maana kwa mapenzi yangu kwao nikaona niandike barua hii nikiamini kuwa ujumbe utafika kwa hadhira.

Nitafurahi kama walengwa ambao ni wasanii pamoja na mashabiki wao watausoma ujumbe huu na kuamua kubadilika kwa ajili ya faida ya jamii inayowazunguuka.

Joseph Kirubo
Chalinze, mkoani Pwani.

Na wewe unaweza kutoa unachokiona, usichopenda katika jamii yako, iwe siasa, uchumi, sanaa na mengineyo kwa kututumia barua fupi kwa emai kambimbwana@yahoo.com au meseji kwa namba +255 712 053949 kisha sisi tutaandika. Pia unaweza kutuma na picha yako kama utaona inafaa na kuwekwa kila Jumamosi.

No comments:

Post a Comment