Pages

Pages

Saturday, July 27, 2013

Msanii wa kizazi kipya, Mady Salu afunga mkanda kulilia ujiko



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Ahmad Salum, maarufu kama Mady Salu, amesema kwamba yupo kwenye mipango ya aina yake ya kumpatia mafanikio.
Msanii Mady Salu akijiachia kama hivyo.
Mady Salu ni kati ya vijana wanne waliotamba na kundi lao la Ngovita Clew lililokuwa na maskani yake Tandale jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuachia wimbo wao wa ‘Maisha Miangaiko’.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mady Salu alisema kwamba kwa sasa amesharekodi wimbo wake wa Tatizo ni ‘Kama Unanipenda’, wimbo aliorekodi katika Studio za BM Records.

Alisema kukamilika kwa wimbo huo ni safari yake ya kutafuta mafanikio katika muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, huku akikumbuka msoto anaoendelea kukumbana nao.

"Nipo sawa katika kutafuta mafanikio ya muziki, maana ndio kipaji change na kazi ninayoipenda sana, hivyo siwezi kuchoka kufanya bidii katika kutunga nyimbo, tangu kusaambaratika kwa kundi letu la Ngovita Clew,” alisema.

Ngovita Clew lilikuwa likiunganisha wasanii kadhaa, akiwamo Gungwa Man, Fico Man, Kijino na Chiteni, ambapo wimbo wao wa kwanza wa Maisha Miangaiko haukuweza kutamba sana licha ya kuwa na mashairi mazuri yenye kujenga jamii bora hapa nchini.

No comments:

Post a Comment