Pages

Pages

Thursday, July 11, 2013

Wakili Peter Kibatala akanusha taarifa za kutekwa na kupigwa

Nikiwa na wakili wa Mume Wangu, Peter Kibatala na mwandishi wa habari Tumaini Makene, ambaye ndio msemaji wa Chadema.

Haya ndio majibu ya wakili wa mume wangu, Henry Kilewo, Peter Kibatala baada ya kudaiwa kutekwa na kupigwa.

Goodmorning: nimepigiwa simu kadhaa toka kwa watu mbalimbali wakinijulia hali baada ya kusoma some post huko Jamii Forum kwamba nimevamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana kuhusiana na case ninazoendesha kuwatetea Wanaharakati kadha wa kadha.

Nawapa pole wote waliostushwa na taarifa hizi.
Ukweli ni kwamba niko salama, nimerudi jana usiku tokea Tabora nilikoambatana na Joyce Kilewo Kiria.

Nitaendelea kufanya kazi zangu kama wakili kwa maadili ya uwakili bila hofu iwayo yote.

Ninasubiri kupangiwa tarehe na Mahakama Kuu kanda ya Tabora kuhusiana na maombi ya marejeo niliyoyawasilisha baada ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora kuwa haina uwezo kutolea maamuzi hoja zetu za kisheria juu ya mashtaka yanayowakabili Henry John Kilewo na wenzake.

Siamini kwamba Tanzania kunaweza kuwa na utaratibu wa kuumiza Mawakili wanaotekeleza majukumu yao ya kisheria. Post hii naitoa toka Mahakama Kuu Dar es Salaam ninakosubiria kuhudhuria case nyingine kwa mujibu wa majukumu yangu ya kila siku.
Viva Freedom.
Peter Kibatala,
Advocate.

No comments:

Post a Comment