Pages

Pages

Thursday, July 11, 2013

Bi Rosemaary Haule, mama yake Profesa Jay adaiwa kufa kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam

Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake. Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'

Mama mzazi wa msanii nguli wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule, maarufu kama Profesa Jay amedaiwa kufariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo na kupeleka huzuni nyumbani kwa msanii huyo, Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.

Bi Rosemary Majanjara Haule, ndio mama wa mwimbaji wa Zali la Mentali, moja ya nyimbo zilizowahi kufanya vyema, huku kichwa cha Jay kikiendelea kubamba katika muziki wa Hip Hop.

No comments:

Post a Comment