Pages

Pages

Thursday, July 11, 2013

Yanga kukipiga na Rhino Rangers leo mjini Tabora



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, leo inaingia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuvaana na timu ya mkoa huo, Rhino Rangers, katika mchezo wa kirafiki, wenye lengo la kuwapatia burudani ya soka mashabiki wao.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto.
Mchezo huo unafanyika siku chache baada ya kutembelea mikoa ya Mwanza na Shinyanga, ambapo pia waliweza kucheza mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara inayotarakiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa mchezo huo utakuwa mwangaza kwa upande wa benchi la ufundi linaloendelea kuinoa timu yao.

Alisema mechi yao ya kirafiki inafanyika huku ikiwa na lengo kubwa la kuwapelekea burudani ya mpira wadau na mashabiki wa soka mkoani Tabora sambamba na ubingwa wao wa Bara.

“Tuliamua kufanya ziara katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora kwa ajili ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara ambapo sisi ndio bingwa mtetezi baada ya kumpoka mtani wetu wa jadi, Simba.

“Mechi ya kesho (leo), itakuwa ya mwisho maana tutarudi jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba nyingine kwa ajili ya kuiweka timu yetu katika mfumo wa ushindani kabla ya kuanza kwa ligi,” alisema.

Yanga inatumia ziara hiyo mikoani kama kushukuru kwa kuungwa mkono, sanjari na kuwaonyesha ubingwa waliotwaa katika msimu wa 2012/2013, ambapo sasa maandalizi yamepamba moto kuanza tena kwa ligi hiyo Agosti 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment