Pages

Pages

Monday, July 08, 2013

Vida: Bado najikongoja ili niwe matawi ya juu kizazi cha Bongo Fleva



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Pili Juma, maarufu kama Vida amesema kuwa bado anajikongoja kuhakikisha kuwa mambo yake yanakuwa mazuri katika kuhakikisha kuwa anatimiza malengo yake.
Msanii kutoka Tanzania House of Talents Vida
Msanii huyo anayetokea katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), alisema kuwa soko la muziki limekuwa na changamoto za aina yake, ila amekuwa makini zaidi katika hilo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Vida anayetokea katika taasisi hiyo iliyoubua na kuendeleza vipaji vya wasanii wengi, alisema sanaa ina changamoto nyingi, hivyo amejipanga kwa ajili ya kutimiza ndoto zake katika tasnia hiyo.

Alisema hata wimbo wake wa Baba Awena, umaendelea kupigwa katika vituo vya redio, japo si kama alivyotarajia, hivyo kusababisha watu wengi washindwe kufahamu ubora wake.

“Namshukuru Mungu kwa kila hatua, hivyo naamini nitaendelea kufanya kazi kwa ajili ya kutangaza zaidi uwezo wangu, maana lengo ni kufikia malengo kama ilivyokuwa kwa nyota wengine,” alisema.

Vida ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaokuja juu katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, huku wimbo wake wa Baba Awena, akiimba na nyota mwingine wa muziki huo, Linex.

No comments:

Post a Comment