Pages

Pages

Monday, July 08, 2013

Habari za picha juu ya ziara ya Edward Lowassa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani, Mheshimiwa Edward Lowassa baada ya kuwasili jijini Mwanza mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Ndege. Anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza kumpokea alipowasili jijini humo.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward lowassa Uwanja, mara baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Selemani Mzee alikuwapo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Edward Lowassa.
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwa ameambatana na makada wa chama, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini Mwanza, wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwa ajili ya mkutano wa muda mfupi ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga hao jijini humo.
Alipowasili alikaribishwa kishupavu na vijana.

No comments:

Post a Comment