Pages

Pages

Monday, July 08, 2013

Azam sasa watamba kuunyakua ubingwa na kuwafanyia umafia Simba na Yanga



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Azam umesema kuwa baada ya kupata udhoefu na kushika nafasi ya pili kwa misimu miwili mfululizo, sasa wanahitaji ubingwa wa Bara ili wapate nafasi ya kuliwakilisha Taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed, alisema kuwa msimu utakaoanza mwezi Agosti mwaka huu, wana kila sababu ya kulitwaa taji hilo.

Alisema kuwa kwa misimu miwili mfululizo, timu yao imeweza kuonysha soka la uhakika na kushika nafasi ya pili, hivyo kwa sasa kila mtu anahitaji kulitwaa taji hilo.

“Hatuoni kwanini mwaka huu tusinyakuwe ubingwa wa Tanzania Bara, maana tayari tumekomaa na tuna uwezo wa juu wa kucheza soka la kuvutia ndani na nje ya nchi.

“Hatuna cha kupoteza kwa sasa, hivyo naamini malengo haya yatafanyika kwa wakati na kulifanikisha, ukizingatia kuwa kama ni ubora Azam tupo katika kundi hilo ndio maana timu zote zinazoshiriki ligi wanapata kazi kubwa kutoka na ushindi katika mechi tunazokutana nazo,” alisema Mohamed.

Baada ya kushika nafasi ya pili katika ligi iliyomalizika hivi karibuni, Azam inayomiliki Uwanja wake wa Chamazi uliopo Mbagala, jijini Dar es Salaam imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

No comments:

Post a Comment