Pages
▼
Pages
▼
Saturday, July 20, 2013
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage atuliza mizuka ya wanachama wake katika mkutano wao uliofanyika Bwalo la Polisi
Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
WANACHAMA wa klabu ya Simba waliokuwa wanataka kuutetemesha uongozi wa mwenyekiti wao Ismail Rage walibaki hoi baada ya kufanyiwa umafia wakati wote wa mkutano huo katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, OysterBay, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Hoja nyingi zilizokuwa zinataka kutolewa na wananchi zilizimwa kibabe na kuwafanya baadhi ya wanachama wapige kelele kuhoji uhalali wa mkutano huo uliofaanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisababisha wanachama wake washindwe kutambua malengo ya mkutano huo licha ya kuibua mgogoro mkubwa katika siku za hivi karibuni miongoni mwa wanachama wake, akimuita Profesa Tolly Mbwete kuzungumzia mikakati ya kimaendeleo ya klabu hiyo, hata hivyo alijikuta akipingwa na wanachama hao waliosema hawataki maneno bali soka.
Hata hivyo, mkutano huo uliingia dosari baada ya kutawaliwa kwa fujo za hapa na pale, ingawa juhudi zilitumika kuzima vurugu hizo kwa kupitia kiti cha Mwenyekiti wao Rage, ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini akitegemea pia jeshi la Polisi.
Awali, mkutano huo ulianza bila ulinzi wa Polisi, lakini alilazimika kuita askari baada ya baadhi ya wanachama kupinga taarifa wa mpango mkakati wa maendeleo ya Simba, hivyo kutishia hali ya usalama ukumbini humo.
Kama kawaida ya Rage, alitumia muda mwingi kuwalanisha wanachama wake hasa wale waliokuwa wakipinga uongozi wake na kuwaahidi kufanya tena mkutano wa dharula hapo mwezi Novemba mwaka huu, pamoja na kuzungumzia pia kuuzwa kwa Emmanuel Okwi nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment