Pages

Pages

Saturday, July 20, 2013

Kodi ya simu ya 1000 kwa mwezi hatihati kuondolewa ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi

KODI ya simu ya shilingi 1000 kwa mwezi, imeendelea kuwa Habari tata kwa Watanzania, huku viongozi wa serikali, wakiwamo wabunge kusimama kidete kuipigania ili iondolewe na kuwafanya wananchi waishi vizuri, huku serikali ikifikiria namna ya kuiondoa.
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, pichani
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, kwa siku kadhaa sasa amekuwa akirushiana maneno katika mitandao na baadhi ya wabunge wa Chadema, akiwamo John Mnyika, mbunge wa Ubungo.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba
Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”

Makamba alisema kuwa wabunge hao ni wanafiki maana wenyewe walikubali ipitishwe, ingawa kwa sasa wameonekana kushikia bango kwa ajili ya kuomba huruma kwa wananchi.

Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, aliizungumzia katika vyombo vya Habari kuwa suala hilo linaangaliwa upya na ikiwezekana itafutwa ili kusitisha mgogoro kutoka kwa wadau wa mawasiliano.

Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.
“Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo,” alisema Mgimwa.

No comments:

Post a Comment