Pages

Pages

Saturday, July 20, 2013

Muumini ajisifia na mipango ya Victoria Sound



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya Victoria Sound, Mwinjuma Muumini,amesema kuwa wamejipanga imara kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kujiweka juu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
Mwinjuma Muumini, Kocha wa Dunia
Victoria Sound bendi iliyoundwa katika siku za hivi karibuni, inachuana vigogo kadhaa vya muziki wa dansi nchini, ikiwamo The African Stars, Twanga Pepeta, inayomilikiwa na Asha Baraka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Muumini alisema hawaoni sababu ya wao kutofikia malengo yao, hasa kutokana na mipango yao kabambe sambamba na mkakati wao kimuziki.

Alisema vijana wake wapo imara kuifanyia kazi kwa mafanikio bendi yao hiyo, akiamini kuwa ndio mpango mzuri wa kuiweka kileleni Victoria Sound katika ramani ya muziki wa dansi.

“Nipo imara katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, huku nikishirikiana na vijana wote wa bendi yetu kwa ajili ya kufanya kazi kwa moyo na kujituma ili iwe njia nzuri ya muziki wetu.

“Tunaamini huo ndio mpango wenye tija katika bendi yetu, hivyo hakuna tunalofanya kwa sasa zaidi ya kutunga nyimbo nzuri, kubuni mitindo yenye ubora katika tasnia ya muziki wa dansi,” alisema.

Kabla ya kuhamia kwenye bendi ya Victoria Sound inayotamba na wimbo wa ‘Shamba la Magugu’, Muumini alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, huku akiwa na uchu wa kuipaisha bendi yake hiyo.

No comments:

Post a Comment