Pages

Pages

Saturday, July 20, 2013

Lady Black akamilisha wimbo wake wa 'Mapenzi Yanakera'



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Felista Magindu, anayetambulika kama Lady Black, amekamilika wimbo wake mpya unaojulikana kama 'Mapenzi Yanakera'.
Msanii wa Hip Hop, Lady Black
Wimbo huo ameurekodi katika Studio za Shinyanga Records, zilizopo mjini Shinyanga, huku akiamini kuwa wimbo huo utamuweka kileleni zaidi katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Shinyanga, Lady Black alisema kuwa wimbo huo umeandaliwa katika kiwango cha juu, hivyo mashabiki wake wajiandaye kupata kitu cha aina yake.

Alisema kuwa wimbo huo hajashirikiana na msanii mkubwa, akiamini kuwa ndio sehemu ya kuonyesha makeke yake katika tasnia ya muziki huo nchini.

“Nimeamua kusimama mwenyewe katika wimbo huo wa Mapenzi Yanakera, nikiamini kuwa ndio jambo muhimu badala ya kuamini kuwa ili wimbo uwe na mvuto lazima wasanii wenye majina washiriki.

“Nimekamilisha wimbo wangu huu niliyourekodi mjini Shinyanga, hivyo mashabiki wangu waendelee kuniunga mkono ili iwe sehemu ya kuniweka juu zaidi katika harakati za muziki huo nchini.

Kwa mujibu wa Lady Black, wimbo wake huo ataanza kuusambaza katika vituo vya redio hapa nchini kwa ajili ya kuwapa fursa mashabiki wake kuusikia na kuelewa zaidi uwezo wake.

No comments:

Post a Comment