Pages

Pages

Monday, July 08, 2013

Watanzania waaswa waichangamkie Country Business Directory



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Country Business Directory, Edson Joel, ameyataka Makampuni, taasisi na ofisi mbalimbali kuchangamkia fursa za matangazo katika directory yao.
Muonekano wa Country Business Directory
Mkurugenzi Mtendaji wa Country Business Directory
Directory hiyo imesheheni vitu mbalimbali vya kusisimua zikiwamo anuani za ofisi za nyingi hali inayoweza kuondolea usumbufu watu katika matukio ya kawaida ya kazi na maisha.
Mkurugenzi wa Masoko wa Country Business Directory Revocatus Mabuye kushoto akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Edson Joel, walipokuwa wanazungumza na Handeni Kwetu Blog ofisini kwao.

Akizungumza katika ofisi zao zilizopo jengo la Quality Centre, Barabara ya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Joel alisema kuwa mradi wao huo utakuwa unatoka kwa mwaka mara moja.

Alisema wamejipanga imara kutoa kitu chenye ubora wa hali ya juu, hivyo kilichopo sasa ni kuwakumbusha Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo zilizopo kwenye Directory yao.

“Tumekuja katika biashara hii tukiwa na dhamira ya dhati ya kutoa huduma nzuri kwa ajili ya kuwapatia watu unafuu wa mtiririko wa kimaisha na majukumu yote ya kikazi.

“Directory yetu inaandaliwa kwa kiwango cha juu na watangazaji wetu wanajua thamani ya kufanya kazi na sisi, hivyo hatuna tunachoweza kusema zaidi ya kuwataka watuunge mkono,” alisema Joel.

Mapema mwaka huu, Joel akishirikiana na wakurugenzi wenzake waliweza kuingiza sokoni Directory hiyo na kusema kuwa imepokelewa kwa mikono miwili na wengi.

No comments:

Post a Comment