Pages

Pages

Wednesday, June 26, 2013

Ziara ya Barack Obama: Tanzania wajivunia kwa fursa za kibiashara



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, amesema ujio wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, utatoa fursa pana za kibiashara kwa Watanzania na kukuza uchumi wao.
 Rais wa Marekani, Barack Obama, pichani, akiwa kwenye mipango ya kuitembelea nchini Tanzania mwishoni mwa wiki hii katika ziara ya kikazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Bernard Membe.
Obama anatarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki hii, huku jiji la Dar es Salaam kwa sasa linatikisika kutokana na kuboreshwa kwa ajili ya ujio huo wa Rais wa Marekani.

Akizungumza leo asubuhi katika redio Clouds, Waziri Membe, alisema sio kweli kuwa Tanzania haunufaiki na ziara ya marais kutoka sehemu mbalimbali za Dunia, hivyo watu wajipange kwa maendeleo.

Alisema kila wanapokuja, kumekuwa na fursa nyingi za kibiashara na uchumi, hivyo wanaamini wale wanaotumia ziara hizo kimaendeleo wanafanikiwa kwa asilimia kubwa.

“Watanzania tujipange kwa maendeleo makubwa baada ya ziara hii ya Obama hapa kwetu, maana faida ni kubwa, ukizingatia kuwa kila wanapokuja huwa kunapatikana fursa za kibiashara,” alisema.

Obama anatarajiwa kuwasili na watu zaidi ya 700, ambapo ziara hiyo imezidi kupokelewa kwa hisia tofauti, huku sehemu mbalimbali za jiji kukiendelea na ukarabati wa kila aina.

No comments:

Post a Comment