Pages

Pages

Tuesday, June 11, 2013

Vibaka maarufu kama Watoto wa mbwa waibuka kwa kasi mkoani Tabora


Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
Na  Mwandishi Wetu (Hastin Liumba),Tabora
PAMOJA na jeshi la Polisi mkoani Tabora,kufanya jitihada za kudhibiti
matukio ya ujambazi mkoani hapa,limeibuka kundi moja hatari ambalo
hujiita “Watoto wa Mbwa.”

Uchunguzi uliofanywa mkoani hapa, umebaini kuwa matendo ya kundi hilo yamerejea upya kama ilivyokuwa miaka ya 1992/1993 likatoweka na kuibuka tena miaka ya 1995/1995,  na sasa limeibuka mwaka huu, hali ambayo ilizua hofu kwa wananchi na mali zao na hasa nyakati usiku.
Aidha kundi hilo linasifika sana kwa uporaji,ubakaji na kujeruhi
wananchi kwenye maeneo mbalimbali ya manispaa Tabora ambapo kuna
kipindi kundi hilo liliwahi kufanya mauaji na kumpora baiskeli askari
wa JWTZ.

Baadhi ya wananchi waliozungumza juu ya hilo walisema kuwa
kundi hilo hufanya uporaji kwenye mitaa mbalimbali ya manispaa Tabora
na mara nyingi hutembea nyakati za usiku wakiwa na silaha za jadi kama
mapanga, visu, nyembe, marungu, fimbo, manati, bisibisi na mawe na huwa wengi takribni vijana zaidi 10.

Aidha makudi hayo huwa matatu hadi manne na hutokea sehemu tofauti
tofauti ndani ya manispaa Tabora wakiwa na malengo ya aina moja ya
uporaji,ubakaji na utesaji.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa “watoto wa mbwa” kama
wanavyojiita,hupora fedha, simu, bidhaa ndogondogo, viatu, nguo baiskeli
na mara kadhaa wamejeruhi na kuacha wananchi kadhaa kwenye ulemavu na wengine kupoteza maisha kwa kipigo endapo watakuwa hawana kitu cha
kumpora mwananchi.

“Hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa la majambazi ambao wamefanya
matukio kadhaa sehemu za minadani na maduka ya M-PESA,ambapo wamefanya uporaji mkubwa mamilioni ya fedha,” walisema.

Baadhi ya taarifa ambazo zimetoka kwa wahanga wa matukio hayo na ndani ya jeshi la polisi,hadi sasa majambazi wameshafanya uporaji wa
mamilioni ya sh minadani na M-PESA wameshaporwa zaidi ya sh 700,000,
500,000  na 200,000 tena kwa milio ya risasi mchana kweupe na majira
ya saa mbili za usiku.

Wananchi kadhaa wamelitupia lawama jeshi la polisi mkoani hapa kwa
kuchelea kila mara matukio yanapotokea huku wakilaumu sana hali ya
amani na usalama wa mali zao kuwa shakani.


No comments:

Post a Comment