Pages

Pages

Monday, June 10, 2013

TCRA waingilia kati kujitoa kwa Star TV kwenye king'amuzi cha Star Times



Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa Star TV kwenye Star Times. Picha kwa hisani ya mtandao...

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),  imeagiza Chaneli ya Star Times irudishwe mara moja kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)

No comments:

Post a Comment