Pages

Pages

Thursday, June 27, 2013

Mohamed Matumla, mtoto wa Snake Boy kuzipiga na Khamis Mohamed, Julai sita, DDC Keko



Mohamed Matumla, pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Mohamed Matumla pichani anatarajia kupanda ulingoni Julai 6 mwaka huu katika Ukumbi wa DDC Keko, kwa ajili ya kupambana na Hamis Mohamed kutoka Gym ya Mzazi.

Akizungumza na mwandishi wetu mwandaaji wa mpambano huo Shabani Adios 'Mwaya mwaya' amesema mpambano huo utasindikizwa na mabondia mbalimbali wanaotamba katika masumbwi.

Mabondia hawo ni Shafii Ramadhani atakayemenyana na Juma Fundi huku Swaleh Mkalekwa akipambana na Cosmas Kibuga, mpambano huo ukitarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.

Huku bondia Mohamed Matumla akimtahadhalisha mpinzani wake kuwa siku hiyo ato kuwa na msalia mtume kwani kawaida yake inajulikana Matumla mpaka sasa amepambana mapambano 13 akidroo matatu na kushinda 10 ata hivyo ame sisitiza kumuhangamiza mpinzani wake mapema kadri iwezekanavyo na kuwaomba wapenzi wa mchezo huo waje mapema kushudia anavyo mmaliza vinginevyo watakosa uhondo wa masumbwi Mbali na kuwepo na mpambano huo Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' atasambaza DVD za mafunzo ya mchezo wa masumbwi

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi.

Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD         mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones, Miguel Cotto, Linox Lewis, David Haye, Mohamed Ali na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .

No comments:

Post a Comment