Pages

Pages

Thursday, June 27, 2013

Kamati ya Utendaji ya Simba kukutana leo jioni Dar es Salaam



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba, leo jioni inatarajia kukutana kwa ajili ya kufanya kikao cha kujadili mambo mbalimbali yanayohusu timu yao, ukiwapo mchakato wa usajili.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.
Simba inakutana huku benchi la ufundi likihaha juu ya mlinda mlango wake, Juma Kaseja, ambaye ameripotiwa kuwa huenda akawa nje ya timu hiyo kwa msimu mwingine wa ligi, japo kocha wa Simba Mkuu, King Abdallah Kibadeni, ameonyesha nia ya kipa huyo abaki kukipiga kwa msimu ujao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangale maarufu kama ‘Mzee Kinesi’, alisema mambo yote yanayohusu klabu yao yatatangazwa kesho Ijumaa na kuiunda timu mpya ya ushindi.

“Kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kusema lolote hadi kikao hiki kifanyike, hivyo hata kama hiyo ripoti au mahitaji ya kocha ingekamilika, bado ingesubiri ridhaa ya Kamati ya Utendaji.

“Kila kitu kimekamilika kwa ajili ya kufanya kikao hicho, huku tukiamini kuwa siku inayofuata, yani Ijumaa yatatangazwa maazimio yanayohusu mchakato mzima wa Simba pamoja na usajili,” alisema.

Simba kwa sasa inayonolewa na King Kibadeni, inafanya mazoezi yake katika Uwanja wa Kinesi, Manzese, jijini Dar es Salaam huku wachezaji mbalimbali wakienda kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

No comments:

Post a Comment