Pages

Pages

Thursday, June 27, 2013

Mgogoro waibuka wa kugombea shule ya Sekondari Ndembela, wilayani Rungwe

 

Na Esther Macha, Mbeya
SAKATA la Mgogoro uongozi shule ya sekondari ya Ndembela ambayo inamilikiwa na Kanisa la Wasabato na wananchi wanaoizunguka shule hiyo uliodumu kwa muda mrefu umechukua sura mpya baada ya uongozi wa serikali wilayani Rungwe kupora vifaa vya shule na kutia kufuri majengo ya shule hiyo huku wakiwataka wamilikiwa kukabidhi majengo hayo kwa wananchi.

Hata hivyo vifaa ambavyo vimechukuliwa na uongozi wa halmashauri ni pamoja nyaraka, Kompyuta,Samani na vyeti vya Wanafunzi .

Akizungumzia tukio hilo Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Brown Osward alisema
kuwa siku ya tukio hilo viongozi mbali mbali wa halmashauri walifika shuleni hapo akiwemo Mwanasheria wa halmashauri ,Ofisa Utumishi pamoja na viongozi wengine wa kata na vijiji kuvamia jengo la utawala kuvunja milango na kubeba vifaa vyote vilivyokuwepo katika majengo hayo ya Utawala.

Aidha Osward alizitaja ofisi ambazo zimevunjwa na vifaa kuchukuliwa ni ofisi ya Mkuu wa shule,uhasibu,taaluma na ofisi inayotunza nyaraka za shule ikiwa ni pamoja na vyeti vya Wanafunzi waliohitimu masomo yao katika shule hiyo.

Akizungumzia tukio Mwenyekjiti wa kijiji cha Ndembela Boaz Mwandambo mvutano wa uongozi wa shule hiyo na wananchi ni muda mrefu kwa kuwa mkataba wa kanisa hilo wa kuendesha shule ulikuwa umemalizika hivyo wananchi walikuwa wanahitaji kurejeshewa majengo yao.

No comments:

Post a Comment