Pages

Pages

Saturday, June 22, 2013

Mambo Fulani Muhimu: Mapenzi ya kweli hayawezi kugawanyika



MAMBO FULANI MUHIMU


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI siku nyingine mimi na mpenzi msomaji wangu tunapokutana katika safu hii ya Mambo Fulani Muhimu, huku nikiamini kuwa utaendelea kuwa pamoja na mimi katika safari hii adhimu.


Hisia kali za mapenzi. Hadi raha.
Ni safari ndefu, huku tukiwa tumeshaugawa mwaka huu tangu tulipoanza siku ya kwanza, yani Januari Mosi, huku safu hii ikiendelea kuungwa mkono kila wiki, jambo linalonipa amani moyoni.

Ni safu ya uhusiano na maisha. Inayohusu mambo ya mapenzi na namna gani ya kuweza kuishi kwa amani na wapenzi wetu, wake au waume, bila kusahau wale waliofanikiwa kufunga ndoa.

Nitakuwa mchoyo wa fadhira kwa wewe unayeguswa na safu hii kiasi cha kuweza kuisoma kila Jumamosi, siku kama ya leo. Nakushukuru sana, maana wewe ni muhimu kwa uwepo wa makala haya.


Tukiachana na hayo, turudi kwenye uwepo wa safu hii, huku leo ikizungumzia zaidi jinsi mapenzi ya kweli yasivyoweza kugawanyika. Yani pale mtu anaposhindwa kuhimili kutoa penzi kwa zaidi ya mtu mmoja.


Ni wazi katika jamii yetu wapo ambao si waaminifu. Baadhi yao hujikuta wakijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na mtu zaidi ya mmoja, ikiwa ni utaratibu usiomuweka huru.


Pamoja na yote hayo, watu aina hiyo, hushindwa kufurahia mapenzi, maana hujikuta wameikosa furaha ndani ya moyo wao. Katika mapenzi, hakuna kitu kizuri kama kujiachia.


Kuona uliyekuwa naye ndio zaidi, hivyo kwa yule mwenye wapenzi wengi hushindwa kuwa huru. Kuna watu ambao wamekubali kujirahisha kwa wanaume au wanawake.


Huyo huyo ana muuza duka, akiamini atakwenda kuchukua vyakula, ama muuza mboga mboga akiamini atapata mboga bure. Pia anaye dereva wa tax, akiamini kuwa atapata hili na lile.


Mtu wa aina hii, amejiwekea huko ni matawi ya kumpa chochote kitu, akiingia kwa makundi ya wasichana wenye tama. Ili tabia hii iendelee, lazima aishi kwa magutu magutu.


Hana amani hata kidogo. Anafanya hivi kwasababu mapenzi hayawezi kugawanyika hata kidogo. Pamoja na kuganga njaa kote, lakini wakati mwingine moyo unahitaji kuwa huru na kufurahia kwa yule uliyemchagua.


Ndio hapo simu inapokuwa nzito. Mtu akimuona mume au mchumba wake, yani aliyemchagua, hujikuta akizima simu maana itamuwekea kauzibe. Watu wa aina hii tunaishi nao mitaani.


Ni wajanja kweli kweli, lakini wanashindwa kujua kuwa siku zote mapenzi ya kweli hayagawanyiki. Mtu anaweza kuwa makini na kujihusisha na mapenzi na kila anayemuona barabarani, lakini si kama hao wote anawapenda.


Zaidi atakuwa amewatamani, hasa kwa wale ndugu zangu wanaochanganywa na vitu vya aina aina, yani wenye tamaa ya vitu vidogo. Wale wanaoona nao wamefikia kuendesha magari ya kuhongwa.


Wale wanaotaka wamiliki simu za bei ya juu kuliko uwezo wao. Hawa wakati mwingine huchezewa kwa kulala kitanda kimoja na midume isiyokuwa ndani ya mioyo yao kwa namna moja ama nyingine.


Pamoja na yote hayo, bado si chaguo halisi la moyo wake. Wakati mwingine hutamani kufurahia zaidi na zaidi na chaguo lake, ila anashindwa, maana ameshawaingiza watu zaidi ya mmoja.


Nadhani katika hili lazima kila mtu ajuwe kuwa ana kila sababu ya kuheshimu moyo wake, kupenda mahali sahihi na kwa wakati sahihi. Mapenzi ya kweli hayagawanyiki.


Kinyume cha hapo ni kujirahisisha tu, jambo ambalo kuna wakati linastahili kuachwa, maana mapenzi ya kweli yana raha yake. 

Nasema hivyo ukizingatia kuwa wanaojihusisha na mapenzi zaidi ya watu wao, hushindwa kufurahia mapenzi, hasa kama hao anaofanya nao si machaguo yao sahihi zaidi ya kushawishiwa na vitu vya kupita.


Huu ni wakati wa kujikita zaidi kwa watu wetu, maana ndio sehemu sahihi na kuacha vitu vya kupita, ukizingatia kuwa bado hatuwezi kufurahia mapenzi zaidi ya kutuacha kwenye wasiwasi wa kimapenzi.


kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087


No comments:

Post a Comment