Pages

Pages

Friday, June 21, 2013

Viongozi wa Chadema walivyoshiriki mazishi ya wahanga wa bomu jijini Arusha

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Grace Kiwelu (Viti Maalum) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Sokoni One, marehemu Judith William Moshi, aliyeuwawa kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho, Jumamosi iliyopita, Juni 15, 2013. Judith alizikwa jana kwenye makaburi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sokoni one, mjini Arusha.

Wabunge wa Chadema wakiwa eneo la makaburi tayari kwa maziko ya marehemu Judith Moshi aliyefikwa na mauti baada ya kulipuliwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha Jumamosi hii.. Marehemu ameacha watoto watatu wa kike.


Naomba radhi kwa picha hii ya tarehe 15 Juni 2013 eneo la Soweto - Arusha.
Kamanda mwenye tisheti nyekundu hapo ni Katibu wa Mbunge Godbless Lema, anaitwa Gabriel Kivuyo yuko ICU kwa siku ya tatu sasa hazungumzi kwasababu aliumia vibaya kichwani na miguu yote haina kazi! Tumuombee Mungu ampe uzima aendelee kulitumikia taifa.

Its so sad kwamba huyo mama aliyelala pembeni yake (akiwa marehemu tayari) baada ya mlipuko Kamanda Judith Moshi ndio amezikwa leo Sokoni Arusha, huku akiwa Katibu wa Chadema katika Kata hiyo. Judith ameacha mtoto wa miaka 2 na watoto wengine wa kike wote!

No comments:

Post a Comment