Pages

Pages

Saturday, June 22, 2013

Simba: Tumemlipa Patrick Liewing Dola 10,000



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Soka ya Simba, jana ilimkabidhi kocha wao wa zamani Patrick Liewig jumla ya Dola 10,000, kwa ajili ya deni lake analoidai timu hiyo, huku akitakiwa kutulia hadi mwezi Octoba kumaliziwa kiasi kilichobaki.
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewing
Liewing aliyekuwa kocha wa Simba, aliwasili nchini kwa ajili ya kudai fedha zake Dola 16,000 ndani ya klabu hiyo, hivyo kulazimika kukaa na viongozi wake wa zamani kwa ajili ya kulimaliza sakata hilo la deni lake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are, maarufu kama mzee Kinesi alisema wamemlipa Liewing kiasi hicho cha fedha.

Alisema uamuzi huo umeafikiwa na pande zote mbili, hivyo wanaamini kocha huyo wa zamani ataridhia na kurudi kwao ama kufanya analohitaji, ukizingatia kuwa tayari wameshamlipa kisheria baada ya mazungumzo yao kufikia pazuri.

“Mapema wiki hii tulizungumza naye na kumtaka atulie ili tumuandalie fedha zake anazodai, ambapo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kumtaka pesa zilizosalia, dola 6000 azipate mwezi 10 mwaka huu.

“Tunashukuru uamuzi huu ameukubali na tayari ameshasaini juu ya uchukuaji huo wa dola 10,000, hivyo tuna amini kwa sasa hakutakuwa na tatizo lolote kati ya Simba na Liewing, aliyekuwa kocha wetu hadi pale ligi ilipofikia tamati,” alisema.

Kocha huyo amekomba pesa zisizopungua 16,450,000 kutoka kwa mabosi wake hao, na kutuliza mzuka kutokana na moto aliokuja nao Tanzania, akigoma kurudi kwao hadi alipwe fedha zake.

No comments:

Post a Comment